Mkufunzi mkuu wa klabu ya Manchester city Pep Guardiola amesema John Stones atakosekana kwa mechi ya usiku wa leo huku akisema Ruben Dias amezidi kuimarika na huenda akashiriki katika mechi ya leo dhidi ya Totenham Hotspers katika dimba la Etihad.
Mkufunzi huyo amesema wachezaji wake bado wanauwezo wa kutetea ubingwa wa ligi licha ya kuwa alama nane nyuma ya vinara wa ligi hiyo Arsenal.
Amesema kwamba kwa sasa ni mapema mno kubaini mshindi wa ligi katikati ya msimu baada ya mechi 18.

