Wazazi eneo la Pwani wamesisitizwa kuhakikisha kuwa wanao wanakumbatia masomo, hasa katika sekta ya ubaharia.
Mwenyekiti wa kamati ya uchumi wa bahari kwenye bunge la kitaifa Kagongo Bowen, amesema kuwa ukosefu wa vyeti katika taasinia hiyo, kwa wananchi wa Pwani ndiyo chanzo cha baadhi ya vijana, kukosa nafasi hizo.
Bowen amedai kuwa idadi kubwa ya wale wanaotuma maombi ya kupata nafasi hizo za ajira, sio wakaazi wa Pwani.
Aidha, ameahidi kuwepo kwa uwazi na haki katika masuala ya ugavi wa ajira kwa wakaazi wa Pwani.

