SERIKALI YASEMA INA CHAKULA CHA KUTOSHA KUSAIDIA WAKENYA WOTE.

“Hakuna mkenya atakaye lala njaa kutokana na ukosefu wa chakula”.

Ni kauli ya waziri wa utumishi wa umma nchini Geoffrey Ruku, ambaye amesema kuwa serikali kuu, imeweka mikakati ya usambazaji wa chakula nchini.

Waziri Ruku amesema mojawapo ya mikakati hiyo, ni kuhakikisha kuwa vyakula vimehifadhiwa vyema, kwenya maghala ya serikali ili kusaidia familia zilizo athirika.

Aidha, waziri Ruku amesisitiza kuwa maeneo yanayo kabiliwa na changamoto za ukame, ikiwa ni pamoja na makaazi rasmi ya wananchi, sawa na taasisi za elimu, zitanufaika na chakula hicho cha msaada.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *