Wito umetolewa kwa wakenya waliopoteza wapendwa wao kufika katika mahakafani ya hospitali kuu ya Malindi kaunti ya Kilifi ili kufanya fanyiwa uchunguzi wa chembechembe za DNA, kubaini iwapo wapendwa wao ni kati ya wale walioangamia katika msitu wa Kwa Binzaro.
Haya ni kwa mujibu wa mshirikishi mkuu wa utawala kanda ya Pwani, Rhoda Onyancha ambaye amesema kuwa zoezi la ufukuzi wa miili kwa sasa limesimamishwa kwa mda baada ya miili 32 kufukuliwa.
Onyacha amesema kuwa kuna baadhi ya miili ambayo haija tambuliwa na wapendwa wao.
Aidha zoezi la upasuaji wa miiili hiyo linatarajiwa kaunza rasmi wakati wowote.

