Katibu wa masuala ya vijana nchini Fikirini Jacobs amewataka vijana kuendelea kujijenga kitaaluma, kisanaa na kibiashara ili kujiimarisha kiuchumi.
Fikirini amesema kuwa kwa sasa serikali ya Kenya kwanza imeanzisha mpango wa kuwasaidia wasanii kupata fedha za kuwasaidia kujiendeleza kiuchumi.
Fikirini amesisitiza vijana kutumia vyema vipaji vyao hasa katika masuala ya sanaa kwani vina uwezo wa kuwainua kiuchumi.
Katibu wa turathi na utamaduni nchini Ummi Bashir, ametoa changamoto Kwa vijana wenye vipaji vya uimbaji kuvitumia kupata riziki badala ya kulalamikia ukosefu wa ajira nchini.

