SERIKALI KUU YAPANIA KUBORESHA MAGEREZA NCHINI.

Kamati ya Bunge la Kitaifa kuhusiana na Utekelezaji wa Katiba (CIOC), imeanza msururu wa ziara za kukagua magereza, kama sehemu ya juhudi pana za kitaifa, kuleta utu na mageuzi ya maana, katika vituo vya kurekebisha tabia.

Katika ziara hiyo, maafisa wa magereza wameibua wasiwasi mwingi, ikiwemo  miundombinu ya zamani, uhaba mkubwa wa sare na mazingira duni ya kazi.

Akizungumza katika gereza la Kilifi, mwenyekiti wa kamati  hiyo Caroli Omondi, ambaye pia ni mbunge wa Suba Kusini kaunti ya Homabay, amesema kuwa, wananuia kugeuza  baadhi ya sheria na  kubuni zingine   za magereza, ili zijumuishwe katika katiba ya mwaka wa 2010.

Aidha, mwenyekiti huyo amedokeza kuwa baadhi ya kesi zimekuwa zikiendeshwa polepole na hivyo kuathiri masuala ya waathiriwa kupata haki.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *