MASHABIKI WA SOKA KURAHISISHIWA VAR

Bodi ya kimataifa ya chama cha soka ya IFAB inayohusika na sheria za kandanda imependekeza kuwepo kwa mawasiliano kwenye viwanja kuhusu uamuzi wa video ili mashabiki wajue kinachojadiliwa na maafisa wa VAR kabla maamuzi kufanyika wakati wa mechi.

Hii inatokana na sintofahamu miongoni mwa mashabiki kila ambapo matukio mbali mbali yanatokea na mwamuzi pekee ndiye anakuwa na uwezo wa kusikia na kufahamu majadiliano na maafisa wanaotazama video kwa maamuzi.

Kulingana na wadau mbali mbali wa soka ulaya wanasema hatua hiyo inafaa kuungwa mkono ili kurahisisha ufahamu kwa mashabiki ambao huenda wakaleta vurugu mechi inapokuwa inaendelea.