Fowadi wa zamani wa klabu ya Arsenal lakini pia Manchester City Emmanuel Adebayor ambaye yupo nchini kwa ziara ya kibiashara amepongeza hatua zilizochukuliwa na serikali ya kenya kurudisha ushwari wa soka hapa nchini muda mchache baada ya marufuku ya soka kuondolewa na shirikisho la soka Fifa.
Alikuwepo uwanjani jana kushughudia mechi ya Tusker dhidi Talanta fc ambayo ilitamatika sare ya mabao 2-2 na kummiminia sifa mlinda lango wa Tusker kutokana na uwezo wake baada ya kutazama mechi hiyo katika dimba la Ruaraka jijini Nairobi.
Raia huyo wa Togo pia ameeleza kusisimuka na uwezo wa talanta zilizoko nchini Kenya akitaja taifa hili kuwa moja ya mataifa yenye uwezo wa kukuza vipaji vya michezo mbalimbali.

