Mkufunzi wa klabu ya Silver Bullets Sammy KARISA anasema kuwa kucheleweshwa kwa kupewa zawadi za governors cup kwa washindi wa mashindano hayo kumewaathiri pakubwa. Anasema wale ambao walikuwa wakiwasaidia kifedha wamejiondoa kutokana na tetesi kuwa walipewa pesa hizo kisiri kaama viongozi.
Anasema yeye kama kocha alikuwepo katika kikosi cha Junju kama mshauri tu wa benchi la kiufundi.
”Mimi nilikuwa katika mashindano ya Governors cup kama mshauri katika kikosi cha Junju. Sasa baadhi ya wachezaji wanalalamika kwamba sisi huenda tulipewa pesa hizo jambo ambalo sio la kweli. Wengine wamejiondoa kikosini, kwa kukata tamaa na kukosa pia kuelewa kuwa bado hela hazijatoka na wanatarajia sisi tuwe zilitufikia. Uwanjani nimesalia na wachezaji 14 pekee wengi waliondoka na wengine wanasusia tu.” Alisema Karisa.
Ameeleza kuwa mashidano ya Governors cup mbali na kuwa yalifanya katika kaunti ya kilifi yamewaletea madhara makubwa hasa kiuchumi. Pia baadhi ya wachezaji katika klabu hiyo wamejiondoa kisa kukosa imani na uongozi wa klabu hiyo.
”Nataka watu wajue kutofautisha kati ya Junju Ward na klabu ya Silver Bullets. Haya mashindano yametuathiri pakubwa mpaka natamani nisingejihusisha. Hivi sasa wale ambao walikuwa wanatusapoti wameanza kutuacha kisa wanasema tulipewa hela na gavana na sio kweli. Tuko na mechi za ugenini Taita Taveta na mpaka sasa hatujajua tutasafiri vipi.” Aliongeza Karisa

