KENYA POLICE FC KUVAANA NA KCB KATIKA FAINALI YA FKF CUP

Kenya Police itakutana na KCB katika fainali ya kombe la FKF mwezi ujao, baada ya kuwalaza AFC Leopards 1-0 katika mechi yao ya nusu fainali.

Mechi hiyo ilichezwa Jumapili alasiri lakini ilisitishwa dakika ya 60 kutokana na sababu za kiusalama baada ya kushuhudiwa vurugu baina ya mashabiki, huku shirikisho hilo likiamuru mchezo wa dakika zilizobaki  30 – uchezwe  kwenye uwanja huo huo, Uwanja wa Police Sacco, Leopards wakilemewa tena katika mechi hiyo

Mechi ya leo iliandaliwa chini ya milango iliyofungwa bila mashabiki uwanjani, na vyombo vya habari pekee viliruhusiwa.

Mshindi wa mechi kati ya Kenya Police FC na KCB atajinyakulia tikiti ya kuwakilisha Kenya katika Kombe la Shirikisho la CAF.