KOMPANY NA HANSI FLICK WAPATA KAZI

Klabu ya Bayern Munich sasa ni rasmi imemthibitisha Vincent Kompany kuwa mkufunzi wao kuelekea siku za usoni katika uhamishounaoingia katika historia ya sokakuwa uhamisho wa kushtukiza.

Vincent Kombani ni kocha wa zamani wa klabu ya Burnley ambayo chini ya Uongozi wake imeshuka daraja kutoka ligi kuu ya uingereza hadi championship.

Kompany mwenye umri wa miaka 38, mchezaji wa zamani wa Manchster City  na amechukua wadhifa wa ukocha Bayern Munich kwenye mkataba utakaotamatika mwezi Juni mwaka 2027.

Klabu ya Barcelona huko uhispania imetangaza  kuwa imemsaini Hansi Flick kuwa kocha mpya wa timu hiyo kwenye mkataba wa miaka miwili.

Hansi Flick sasa anachukua mikoba ya kocha Xavi Hernandes kama mkufunzi mpya baada ya kufutwa siku ya ijumaa.

Hansi Flick mwenye umri wa 59 ambaye ni kocha wa zamani wa klabu ya Bayern Munich kule Ujerumani aliwasili Barcelona jana kusaini mkataba wake rasmi.

Taarifa zinasema kwamba nia ya Xavi ya kumuuza mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski mwenye umri wa miaka 35 msimu huu ilikuwa sababu kuu ya Mhispania huyo kufukuzwa kazi Barcelona mwezi huu.