FIRAT ANASEMA KIKOSI KIKO TAYARI

Mkufunzi mkuu wa timu ya taifa ya Harambee Stars Engin Firat amesema kwamba kikosi chake kiko imara  kwa ajili ya mashindano ya kutafuta tikiti ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2026 kipindi hiki cha likizo ya soka kimataifa.

Harambe Stars watakuwa wanasafiri wikendi hii kwenda Malawi ambako mechi za nyumbani watachezea kutokana na Kenya kuwa bila viwanja tayari vya hadhi ya kimataifa kulingana na waandalizi.

Harambe stars wanatarajiwa kushuka dimbani dhidi ya Burundi kisha kukipiga dhidi ya mabingwa wa Afcon mwaka huu Ivory Coast.

Hata hivyo Engin Firat amehakikisha kwa wakenya kuwa Michael Olunga atakuwepo katika mashindano hayo baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa huenda akawa ametemwa kimakusudi na kocha huyo.

Firat amesema kuwa Olunga pamoja na wenzake Richard Odada na Daniel Anyembe watajiunga na kikosi huko Malawi kutokana na sasa bado hawajafika Kenya