Straika wa timu ya taifa ya Uruguay Edison Cavanani amestafu rasmi soka kimataifa baada ya kutumika timu yake ya taifa kwa takriban miaka 14.
Cavani mwenye umri wa miaka 37 ameifungia timu yake ya taifa mabao 58 katika mechi 136 na katika huduma yake aliisaidia Uruguay kushinda kombe la Copa America mwaka 2011.
Kwa sasa Cavani anachezea Boca Juniors baada ya kuchezea vilabu kadhaa vikubwa Ulaya ikiwemo PSG, Napoli pamoja na Manchester United
Winga wa timu ya taifa ya Argentina Angel Di Maria ni rasmi sasa atakuwa anajiunga na klabu ya Inter Miami ya Marekani baada ya kuachiliwa na klabu yake ya sasa Benfica.
Hii ni baada ya kandarasi yake na Benfica kutamatika rasmi majira haya ya kiangazi. Di Maria sasa anaungana na nyota mwenza wa Argentina Lionel Messi pamoja na Luis Suarez katika klabu hiyo mpya ya Inter Miami.

