‘Shirikihso la soka la FKF mjini Malindi limetangaza kuwa vilabu ambavyo vitakuwa havijakamilisha malipo ya kushiriki katika ligi ya eneo bunge hilo huenda ikatolewa kabisa kwenye ligi.
Hii ni kulingana na mwenyekiti wa tawi hilo Tom Lango ambaye ameambia Tama La Spoti kuwa wanalenga kutumia hela hizo kuwazawidi wachezaji mwisho wa msimu.
Anaseka kikao hicho kitakachofanyika wikendi ijayo mjini Malindi kina lengo la kujadili masuala mengine pia ya changamoto za ligi lakini ajenda kubwa kwasasa ni fedha za kuendesha ligi hiyo
”Kikao hicho tutajadili mambo mengi kuhusu suala la hizo fedha. Lazima timu zilipe ili mwisho wa msimu tupate pesa zawadi” Alisema Tom Lango
Tom ameweka bayana kuwa mbunge wa Malindi Amina Mnyazi mwaka jana aliwafeli kwenye kupeana zawadi licha ya kuwa alikuwa amewaahidi wachezaji kuwa angefanya hivyo mwisho wa msimu.
”Msimu uliopita mbunge Amina Mnyazi alitufeli ndio maana sasa tunajipanga wenyewe tu. Kwa hivyo timu zilipe na sisi mwisho wa msimu tuwazawidi.” Aliongeza Lango.

