ALIYEKUWA GAVANA WA KIAMBU FERDINAND WAITITU AKATA RUFAA DHIDI YA HUMU YA MIAKA 12 GEREZANI.
Aliyekuwa Gavana wa kaunti ya Kiambu Ferdinand Waititu, amewasilisha rufaa ya kupinga uamuzi wa kumhukumu kifungo cha miaka 12 jela kutokana na kesi ya ufisadi ya Shilingi milioni 588. Katika nakala zake alizowasilisha katika Mahakama Kuu ya Kupambana na Ufisadi Milimani, kupitia wakili wake Danstan Omari, Waititu amemkashifu hakimu Thomas Nzyoki, kwa kutochanganua kikamilifu ushahidi […]



