VIONGOZI WA KAUNTI YA TANA RIVER WATAKIWA KUSHIRIKIANA.

Kuna haja ya viongozi wa serikali ya kaunti ya Tana River kushirikiana katika kutatua changamoto ya utumizi mbaya wa fedha za umma katika kaunti hiyo.

Ni kauli ya Seneta wa kaunti ya Tana River, Danson Mungatana ambaye amesema kuwa hatua hiyo itasaidia pakubwa katika kuboresha shughuli za utendakazi wa serikali ya kaunti hiyo.

Mungatana amesema kuwa licha ya kaunti hiyo kukubwa na changamoto ya utumizi wa fedha, umoja huo utasaidia kuchunguza jinsi ambavyo fedha za kaunti hutumika.

Wakati uo huo spika wa bunge la kaunti ya Tana River, Osman Galole amesema kuwa seneta huyo atakuwa akihutubia bunge hilo kuhusiana masuala mbali mbali mara moja baada ya miezi mitatu ama minne mwaka huu.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *