MBUNGE WA MALINDI KAUNTI YA KILIFI AMINA MNYAZI AORODHESHWA KATI YA WABUNGE 50 BORA NCHINI.

Wakaazi wa Malindi kaunti ya Kilifi wamepongeza utafiti wa kampuni ya Infortack ambao umemuorodhesha mbunge wa Malindi Amina Mnyazi kati ya 50 bora katika taifa hili.

Mnyazi alipata asilimia 58 ya utendakazi bora katika taifa hili, utafiti ambao ulizingatia pakubwa utumizi wa fedha za hazina ya NG-CFD katika eneo bunge hili la Malindi.

Kulingana na wananchi hao wakiongozwa na Steven Mlanda na Florence Ngowa wamempongeza kiongozi huyo kutokana hatua ya kuendeleza haki na usawa hasa katika shughuli za ugavi wa fedha za basari nchini.

Wakizungumza katika zoezi la utathmini wa ardhi ya ujenzi wa soko la Kisasa katika eneo la Msabaha, wamemtaka kiongozi huyo kuendeleza jitihada zaidi katika kufanikisha miradi ya maendeleo kwa wananchi wake.

Kauli hizo zimeungwa mkono na mmoja wa viongozi wa kijamii eneo hilo Mohammed Mrefu, ambaye amesema kuwa mbunge huyo hajakuwa akizembea katika kuhudumia wananchi wake.

Aidha utafiti huo ulibaini kuwa Mbunge Embakasi Mashariki kaunti ya Nairobi Babu Owino ndiye kiongozi bora zaidi katika bunge la kitaifa humu nchini akifuatiwa kwa karibu na mbunge wa Kiharu kaunti ya Nyeri, Ndindi Nyoro.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *