ALIYEKUWA GAVANA WA KIAMBU FERDINAND WAITITU AKATA RUFAA DHIDI YA HUMU YA MIAKA 12 GEREZANI.

Aliyekuwa Gavana wa kaunti ya Kiambu Ferdinand Waititu, amewasilisha rufaa ya kupinga uamuzi wa kumhukumu kifungo cha miaka 12 jela kutokana na kesi ya ufisadi ya Shilingi milioni 588.
Katika nakala zake alizowasilisha katika Mahakama Kuu ya Kupambana na Ufisadi Milimani, kupitia wakili wake Danstan Omari, Waititu amemkashifu hakimu Thomas Nzyoki, kwa kutochanganua kikamilifu ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka.

Mawakili wa Waitutu wameaeleza sababu kadhaa za kukata rufaa, ambazo ni pamoja na madai kwamba, upande wa mashtaka ulishindwa kufikia kiwango cha uthibitisho unaohitajika, mahakama ya mwanzo ilipuuza utata katika kesi ya mwendesha mashtaka, na mashahidi wakuu hawakuitwa kutoa ushahidi.

Mawakili hao wanadai kuwa mahakama ilikosa kuthamini ukinzani katika ushahidi uliowasilishwa, jambo ambalo lilizua shaka kuhusu kuhusika kwake katika madai ya uhalifu.