WATALII ELFU MOJA WAWASILI ENEO LA PWANI KUPITIA BANDARI YA MOMBASA.

Huenda sekta ya utalii eneo la Pwani ikaboreka hata zaidi, baada ya jumla ya watalii elfu moja, kuwasili katika Ukanda huu kupitia bandari ya Mombasa.

Akithibitisha hilo, mkurugenzi mkuu wa bandari ya KPA mjini Mombasa nahodha William Ruto, amesema kuwa wapo tayari kupokea meli nyingi zaidi, zilizo na watalii wengi wakao saidia uchumi wa eneo hili kuboreka.

Akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa wamiliki wa mahoteli katika eneo hili la Pwani, watanufaika pakubwa na ujio wa watalii hao.

Kwa upande wake mmoja wa wafanyakazi wa bodi ya utalii nchini Wausi Walya, ameunga mkono kauli hiyo huku akisema kuwa kuboreka kwa mapato ya wakenya, kutokana na ujio wa watalii wengi wanaozuru maeneo mbali mbali ya Ukanda huu wa Pwani.
……….TAYARISHA TWO………..