HABARI

SAMUEL TEMO KUJIUNGA NA MALINDI PROGRESSIVE ACADEMY

Huenda Temo Samuel, mchezaji wa zamani wa klabu ya Furunzi Fc akajiunga na klabu ya Malindi Progressive Academy pindi tu atakapoachana na Mombasa Elites klabu inayoshiriki katika ligi ya Kitaifa ya Super League. Nyota huyo amekuwa akisusia kujihusisha tena na klabu  hiyo ya Mombasa kutokana na kile anachokitaja kuwa Mombasa Elites imeshindwa kutimiza makubaliano ikiwemo […]

SAMUEL TEMO KUJIUNGA NA MALINDI PROGRESSIVE ACADEMY Read More »

BEACH BAY FC YALIA

Klabu ya Beach Bay inayoshiriki katika ligi ya daraja la pili kitaifa kutoka eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi inalilia udhamini ili kufadhili mechi zake. Kulingana na MKufunzi James Mkutano ni kuwa ukata wa kifedha ni kati ya changamoto zinazowakabili kwa sasa jambo ambalo ana hisi limekuwa likivunja morale wachezaji wake. Mkutano ametuma wito

BEACH BAY FC YALIA Read More »

HII NDIO SABABU SUPERSPORT HAITAONYESHA AFCON

Supersport ambao wanaongoza katika upeperushaji wa habari za michezo ya kimataifa hasa soka wametangaza rasmi leo kuwa hawatakuwa wakipeperusha moja kwa moja mashindano ya Afcon yanayoanza tarehe 13 mwezi huu wa Januari. Wamiliki Multichoice wametoa taarifa leo kuwa kukosa ruhusa ya kupeperusha matangazo hayo ndio chanzo kikubwa cha kutotangaza soka hilo kubwa la bara afrika.

HII NDIO SABABU SUPERSPORT HAITAONYESHA AFCON Read More »