SAMUEL TEMO KUJIUNGA NA MALINDI PROGRESSIVE ACADEMY

Huenda Temo Samuel, mchezaji wa zamani wa klabu ya Furunzi Fc akajiunga na klabu ya Malindi Progressive Academy pindi tu atakapoachana na Mombasa Elites klabu inayoshiriki katika ligi ya Kitaifa ya Super League.

Nyota huyo amekuwa akisusia kujihusisha tena na klabu  hiyo ya Mombasa kutokana na kile anachokitaja kuwa Mombasa Elites imeshindwa kutimiza makubaliano ikiwemo malipo na marupurupu yake kwa muda.

Kwa sasa amekuwepo nyumbani kwao Msabaha ambako amekuwa akishiriki mazoezi na klabu hiyo huku akionyesha kuwa angependa kufanya kazi tena na mkufunzi Nero Chishenga ambaye washawahi kufanya kazi pamoja kwenye zama za Furunzi Fc katika ligi ya daraja la pili.