Shirikisho la soka barani Afrika CAF limeongeza hela za kushindaniwa katika makala ya kombe la Afcon mwaka huu yatakayofanyika nchini Ivory Coast kwa asilimia arubaini.
Mwaka huu bingwa wa kombe la Afcon atakwenda nyumbani na dola za kimarekani milioni 7 sawa na Bilioni 1.1 za Kenya huku nafasi ya pili akijishindia dola milioni 4 sawa na milioni 632 za Kenya.
Timu yoyote ya kutonga semi fainali ni dola milioni 2.5 huku wale watakao faulu kuingia robo fainali ni dola milioni 1.7
Kulingana na rais wa Caf Patrice Motsepe ni kuwa shirikisho la soka la bara hili la Afrika limepiga hatua kubwa za kimaendeleo jambo ambalo limepelekea kuongezeka kwa hela za ushindani katika mashindano yote ya CAF hasa makala ya 34 ya Afcon yatakayofanyika mwaka huu.

