Msambuliaji wa zamani wa klabu ya Manchester United Wayne Rooney amesema kwamba hajakata tamaa kwenye azma ya kuwa mkufunzi bora zaidi ulimweguni.
Amesema haya kwenye mahojiano na Sky Sport siku chache baada ya kupigwa kalamu na timu ya Birmingham city ya daraja la pili ya Uingereza ambapo alikua mkufunzi wa timu hiyo kwa siku 83 pekee.
Alifurushwa kuwa mkufunzi wa timu hiyo baada ya kuandikisha matokeo duni kwenye mechi 15 alizochezesha na kuifanya timu ya Birmingham kushuka hadi nambari ya 20 kwenye jedwali ya ligi hiyo.
Kulingana naye amesema kufutwa kwake bado hakuja mkatisha tamaa bali anachukua muda kidogo kuchunguza ni wapi alipokosea kama mkufunzi ili kujiboresha zaidi katika mbinu zake kama mkufunzi.
Rooney Ambae alianza safari yake ya kua mkufunzi Agosti mwaka wa 2020 alipotangazwa kuwa meneja wa timu ya uingereza katika soccer aid mwaka huo.akisaidiwa na sam allardyce na kocha wa makipa david seaman.
Kisha baadae mwaka huo wa 2020, alichaguliwa kuwa mkufunzi wa derby county baada ya kocha wa timu hiyo Philip cocu kufurushwa ambapo rooney alichukua usukani huo ingawa hakuwa na mafanikio mazuri kama alivyo tarajiwa, jambo ambalo lilifanya timu hiyo kushushwa taraja nae mkufunzi Rooney akamua kujihuzuli tarehe 24 june 2022 kama meneja wa timu hiyo.
Wiki chache baada ya kujihuzulu, huduma zake zilihitajika na klabu yake ya zamani ya MLS ,D.C.United ambapo alipata pointi 9 kati ya mechi 14 za mwisho alizochezesha kama mkufunzi.
Rooney alilazimika kuregea tena uingereza octoba tarehe 11 ,2023 kama mkufunzi wa Birmingham city kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu.
kati ya siku 83 alizokuwepo kwenye klabu hiyo alichezesha mechi 15 na kufanikiwa kushinda mechi mbili pekee jambo lililopelekea kupigwa kalamu kwa mara nyengine tena.
Kwa sasa Rooney ambaye anashikilia rekodi ya kuwa mshambuliaji bora zaidi wa timu ya Manchester United kwa kufunga mabao 253 na kuzalisha magoli 103 amesema bado yupo sokoni kuona kwamba kuna mahali kwengine ambapo atahitajika ili kuendeleza azma hiyo ya kuwa mkufunzi bora zaidi ulimwenguni.
Je wadhani anauwezo wa kufanikiwa kwenye safari yake ya kua mkufunzi bora ama aweze kustaafu kwa mambo ya soka ?

