IEBC YATAKIWA KUWAKABILI WANASIASA WANAOPANGA KUHARIBU MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2027.
Chama cha DCP kimeitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC, kuwachukulia hatua kali za kisheria, wanasiasa wanaoendeleza semi za kuwa na mipango ya kushiriki wizi wa kura za urais mwaka 2027. Naibu kinara wa chama hicho Cleophas Malala, amesema kuwa watawasilisha ombi kwa tume hiyo, kuhusiana na suala la kukabili kisheria wanasiasa hao. […]



