Rais William Ruto amewataka wakenya kujitenga na siasa za ukabila na badala yake kupigia debe umoja na mshikamano ya kitaifa.
Akizungumza katika eneo la Embakasi kule kaunti ya Nairobi, Ruto amesema kuwa atahakikisha wakenya katika kila jamii kote nchini, wanashirikishwa katika masuala ya maendeleo.
Kiongozi wa taifa ameelezea kuwa migawanyiko ya kikabila, ndiyo chanzo cha kushuhudiwa kwa mizozo kati ya wananchi kwenye jamii.
Wakati huo huo amesisitiza wananchi kujitenga na viongozi wanaodaiwa kutumia vijana, kusababisha vurugu katika maeneo tofauti ya taifa hili.

