WATUMISHI WA UMMA WAONYWA DHIDI YA KUCHELEWA KAZINI.

Waziri wa utumishi wa umma nchini Geoffrey Ruku, amewaonya maafisa wa serikali dhidi ya kuchelewa kufika kazini, akisema kuwa huenda wakaadhibiwa.

Akizungumza baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika afisi za umma kule kaunti ya Nyeri, waziri Ruku amesema kuwa hatua hiyo, imechangia wananchi kutopata huduma bora kutoka kwa serikali kupitia afisi hizo.

Ameongeza kuwa hatua hiyo, imechangia wananchi wengi kutilia shaka utendakazi wa rais William Ruto kitaifa.

Aidha, ameagiza hatua za kinidhamu kuchukuliwa dhidi ya watumishi wa umma, waliokosa kufika kazini kwa wakati unaofaa  kaunti hiyo ya Nyeri.