Idara ya usalama nchini imeapa kuwachukulia hatua za kisheria wanasiasa watakaopatikana na hatia, ya kufadhili maandamano ya kizazi cha Gen Z katika maeneo tofauti ya taifa hili.
Katika taarifa wa waandishi wa habari, kwenye majengo ya afisi za wizara hiyo kaunti ya Nairobi, Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen, amekashifu hatua ya waandamanaji kuharibu mali ya wananchi wasio na hatia.
Murkomen amesema kuwa licha ya wakenya kuwa na haki ya kushiriki maandamano, hakuna aliye na ruhusa ya kuharibu mali ya mwengine.
Vile vile amesema kuwa afisaa yeyote wa polisi aliyepatikana na hatia ya utumizi wa nguvu kupita kiasi wakati wa maandamano, atakabiliwa kwa mujibu wa sheria za taifa.
Aidha, waziri huyo ameahidi kutoa agizo kwa maafisa wa polisi kuhusiana na jinsi wanavyopasa kutumia silaha zao.

