SERIKALI YA KAUNTI YA TAITA TAVETA YAANZISHA MIKAKATI YA KUKABILIANA DHULMA ZA KIJINSIA.

Kufuatia ongezeka la visa vya dhulma hasa kwa watoto na wanawake kaunti ya Taita Taveta, serikali ya kaunti hiyo imeandaa kongamano la kujadili mbinu za kukabili suala hilo mjini Voi.

Gavana wa kaunti hiyo Andrew Mwadime, amesema kuwa visa vya dhulma za kijinsia hasa kwa wanawake na watoto kaunti ya Taita Taveta, vimeendelea kukithiri kila uchao kaunti hiyo.

Mwadime ameelezea kuwepo kwa asilimia ndogo ya visa vya wanaume wanao dhulumiwa kwenye jamii.

Kauli yake imeungwa mkono na naibu gavana wa kaunti hiyo Christine Kilalo, ambaye ameelezea kuwa na ushahidi wa visa hivyo huku akitoa wito kwa jamii, kushurikiana na wadau mbali mbali ili kukabiliana na dhulma hizo kwenye jamii kaunti ya Taita Taveta.

Aidha, waziri wa masuala ya vijana katika kaunti hiyo Shedrack Mutungi, amesisitiza kubuniwa kwa mikakati ya jinsi ya kukabiliana na visa vya dhulma za kijinsia kwenye jamii.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *