Jumla ya taasisi 7,446 za afya kitaifa, zimepokea mgao wa jumla ya shilingi bilioni 51.3, kutoka kwa serikali ya kitaifa kupitia mpango wa mamlaka ya SHA, ili wakenya wanufauike na bima ya afya SHIF.
Kulingana na waziri wa afya nchini Aden Duale, hatua hiyo itasaidia pakubwa katika kuboresha huduma za afya kwa wakenya, ambao wamesajiliwa kwenye bima hiyo mpya.
Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari jijini Nairobi mda mfupi uliopita, Duale amewataka waajiri kuhakikisha kuwa wanatekeleza wajibu wa kulipia wafanyakazi wao ada hitajika kwa mamlaka hiyo ya SHA.
Duale amesema kuwa kufikia sasa, zaidi ya vituo mia saba vya afya, hasa vya kibinafsi zimefungwa kutokana na hatua ya kutoafikia vigezo hitajika ili kuendeleza shughuli za kutoa huduma za afya kwa wakenya.

