Kitaifa

SERIKALI KUU YAAHIDI KUKAMILISHA DENI LA SHULE ZA UPILI ZA UMMA.

Wizara ya elimu nchini imewahakikishia walimu wakuu katika shule za upili za umma, kuwa watapokea deni lao la shilingi bilioni 14, za muhula huu wa kwanza wiki hii. Waziri wa elimu Julius Ogamba Migosi, amesema kuwa fedha hizo ni asilimia 25 ya jumla ya pesa ambazo, taasisi hizo zilitarajiwa kupokea katika muhula huu wa kwanza. […]

SERIKALI KUU YAAHIDI KUKAMILISHA DENI LA SHULE ZA UPILI ZA UMMA. Read More »

WATALII ELFU MOJA WAWASILI ENEO LA PWANI KUPITIA BANDARI YA MOMBASA.

Huenda sekta ya utalii eneo la Pwani ikaboreka hata zaidi, baada ya jumla ya watalii elfu moja, kuwasili katika Ukanda huu kupitia bandari ya Mombasa. Akithibitisha hilo, mkurugenzi mkuu wa bandari ya KPA mjini Mombasa nahodha William Ruto, amesema kuwa wapo tayari kupokea meli nyingi zaidi, zilizo na watalii wengi wakao saidia uchumi wa eneo

WATALII ELFU MOJA WAWASILI ENEO LA PWANI KUPITIA BANDARI YA MOMBASA. Read More »

ALIYEKUWA GAVANA WA KIAMBU FERDINAND WAITITU AKATA RUFAA DHIDI YA HUMU YA MIAKA 12 GEREZANI.

Aliyekuwa Gavana wa kaunti ya Kiambu Ferdinand Waititu, amewasilisha rufaa ya kupinga uamuzi wa kumhukumu kifungo cha miaka 12 jela kutokana na kesi ya ufisadi ya Shilingi milioni 588. Katika nakala zake alizowasilisha katika Mahakama Kuu ya Kupambana na Ufisadi Milimani, kupitia wakili wake Danstan Omari, Waititu amemkashifu hakimu Thomas Nzyoki, kwa kutochanganua kikamilifu ushahidi

ALIYEKUWA GAVANA WA KIAMBU FERDINAND WAITITU AKATA RUFAA DHIDI YA HUMU YA MIAKA 12 GEREZANI. Read More »