WAFUASI WA ALIYEKUWA WAZIRI WA JINSIA NA UTAMADUNI AISHA JUMWA WAPONGEZA UTEUZI WAKE KWENYE BODI YA BARABARA NCHINI.
Baadhi ya wandani wa mwanasiasa Aisha Jumwa wamepongeza hatua ya rais William Ruto kumteua kiongozi huyo kuwa mwenyekiti wa bodi ya barabara humu nchini. Wakiongozwa na Abdrahman Omar, wamemtaja Rais Ruto kuwa kiongozi ambaye anayejali wakaazi wa kaunti za Pwani kutokana na hatua yake kumteua Jumwa kwenye wadhifa huo. Wakizungumza na wanahabari hapa mjini Malindi […]



