Gavana wa kaunti ya Mombasa, Abdulswamaad Sharrif Nassir amekashifu vikali hatua ya mkaguzi mkuu wa bajeti Magaret Nyakang’o kuwataja magavana nchini kusitisha shughuli za utoaji wa basari.
Kwa mujibu wa Shariff, serikali za kaunti zinapaswa kupewa nafasi ya kutumikia wananchi wake hasa katika masuala ya kufadhili elimu ya wanafunzi wanaotoka familia zisizo kuwa na uwezo mzuri wa kifedha.
Akihutubua umma katika kaunti ya Mombasa, gavana Nassir amesema kuwa idadi kubwa ya wazazi katika taifa hili wanakabiliwa na changamoto za kifedha na hivyo kuna haja ya wao kusaidiwa katika kuwalipia wanao karo.
Aidha amemtaka mkaguzi mkuu wa bajeti Margaret Nyakang’o kukoma kuingilia kati utendakazi wa serikali za kaunti nchini.

