VILABU VINNE VYA SOKA MAGARINI VYATIMBA LIGI YA KAUNTI

Vilabu vinne vya soka eneo bunge la Magarini  vimepanda daraja hadi ligi ya kaunti ya Kilifi baada ya kuandikisha matokeo mazuri msimu uliopita.

Klabu ya Lubumbashy ambayo ilishinda ubingwa wa mashindano ya Mini League mwaka jana, klabu ya Evergreen, Wakala City lakini pia Danforce ya Marafa ndio klabu zilizoingia katika ligi ya kaunti.

Kulingana na waraka uliochapishwa mitandaoni na ofisi ya fkf tawi la eneo bunge hilo na kutiwa sahihi na katibu mkuu Emmanuel Kazungu, waraka huo umethibitisha kwamba wa sasa vilabu hivyo vinne vimeshinda vigezo vyote vya kupanda daraja.

Ligi ya kaunti huenda ikaanza mwishoni mwa mwezi huu wa Januari kwa msimu wa 2022/2023.