Mkufunzi mkuu wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp amesema hana mpango wa kuondoka klabu hiyo kwa hivi sasa pamoja na kwamba timu hiyo imekuwa haifanyi vizuri.
Kocha huyo raia wa Ujerumani amesema anaweza kuondoka tu Liverpool kama atalazimishwa kufanywa hivyo lakini vinginevyo hana huo mpango.
Maneno hayo yanatokea kwenye kipindi ambacho Liverpool wanashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa EPL alama 10 pungufu kuingia nne bora.
Liverpool usiku wa leo imefuzu kuingia katika hatua ya raundi ya nne katika soka la FA baada ya kusajili ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Wolveshamption ugenini.

