FKF KUPEANA MAFUNZO YA SOKA KWALE KABLA MSIMU MPYA KUANZA

Hamisi Mwakoja ambaye ni mwenyekiti wa shirikisho la soka kaunti ya Kwale anasema ligi ya kaunti hiyo itaanza rasmi mwezi February mwaka huu katika msimu wa mwaka 2022/2023.

Kwa sasa matayarisho ya msimu huo yanaendelea na shirikisho la soka linalenga kufanya kikao na wakuu wa vilabu tarehe 26 mwezi huu ili kupanga mikakati ya kuendesha msimu ujao.

Uhaba wa marefa katika kaunti hiyo ni kati ya changamoto kubwa inayokumba soka la Kwale jambo ambalo limepelekea shirikisho la soka la FKF tawi la kaunti hiyo kulenga kufanya mafunzo ya waamuzi pamoja na kufunza wakufunzi wa vilabu sheria za soka kama njia moja ya kuboresha soka la mashinani.