Klabu ya Arsenal imebashiriwa kushinda ligi ya msimu huu wa mwaka 2022/2023 na Supercomputer za kampuni ya FiveThirtyEight.
Hii ni baada ya mabingwa watetezi Manchester City kupoteza mechi yao ya ligi wikendi ilopita dhidi ya Manchester United kwa kichapo cha mabao 2-1 huku viongozi wa ligi hiyo Arsenal kushinda mechi yao dhidi ya Tottenham Hotspers kwa mabao 2-0.
Supercomputer hizo zimebashiri kwamba Arsenal itashinda ligi kwa alama 85 huku Manchester City wakipoteza ubingwa wao kwa kumaliza ligi na alama 82. Manchester United na Newcaste United ndio klabu zitakazomaliza katika nne bora.

