JAMAA AFIKISHWA MAHAKAMANI MJINI MALINDI KWA KOSA LA ULAWITI

Jamaa mmoja mwenye umri wa miaka 28 amefikishwa mahakamani hapa mjini Malindi kwa kosa la kuwalawiti watoto zaidi ya wawili katika eneo la Kisumu ndogo kati ya tarehe mosi Agosti mwaka jana na januari ya mwaka huu.
Upande wa mashtaka umesema kuwa jamaa huyo kwa jina Mbauni Muriithi aliwahadaa wazazi wa watoto hao wa kiume walio kati ya umri wa miaka 11 kuwa alikuwa anawashirikisha na soka ila idara ya upelelezi ilibaini kuwa mshtakiwa alikuwa akiwadhulumu wavulana hao kwa kuwalawiti.
Jamaa huyo ambaye alikamatwa tarehe 11 mwezi huu wa januari amepinga mashtaka hayo mbele ya jaji Elizabeth Usui.
Jaji Elizabeth amehoji kuwa mahakama itatoa mwelekeo zaidi  tarehe saba mwezi ujao mwaka huu baada ya kupokea ripoti kutoka kwa wakili wa mshtakiwa.