Klabu ya Young Bulls inayoongozwa na mkufunzi Ali Said Gaucho inazidi kuandikisha matokeo yasioridhisha hasa katika mechi za ugenini kulingana na mashabiki wao.
Jana ilipiga sare ya bao 1-1 dhidi ya Zetech Titans katika uwanja wa Gems Cambrige jijini Nairobi.
Kukosekana kwa matokeo mazuri katika klabu hiyo kunadhidirika hasa baada ya mshambuliaji wao matata Alex Mwalimu ambaye amekaa nje kwa muda kutokana na jeraha alilopata katika mechi ya derby dhidi ya klabu ya Malindi Progressive.
Mshambuliaji huyo mkazi wa Matsangoni kaunti ya kilifi msimu huu katika ligi ya daraja la kwanza amefunga mabao 11 akiwa na Young Bulls.

