MKUFUNZI WA SPARKI YOUTH AWASUTA ‘WENYE VILABU’

Mkufunzi mkuu wa klabu ya Sparki Youth kutoka kaunti ya Mombasa ametoa wito kwa wakuu wa vilabu vya daraja la chini kuwa na subra na makocha wa vilabu vyao ili wawe na wakati mzuri wa kuunda vikosi.

Akizungumza na Tama La Spoti kupitia njia ya simu mkufunzi Abdala amesema kwamba baadhi ya viongozi wanatamaa ya mafanikio ya haraka kwa vilabu vyao tofauti na jinsi kulivyo na ugumu katika soka la mashinani.

Hayo yanajiri baada ya mkufunzi wa klabu ya Furunzi fc Nero Chishenga kujiuzu kutoka uongozi wa klabu hiyo baada ya kuwepo na migogoro ya mara kwa mara.

Mkufunzi Nero alijiondoa katika majukumu ya Furunzi klabu inayoshiriki katika ligi ya daraja la pili kitaifa na sasa ameanza kazi mpya ya kuwafunga soka vijana wa klabu ya Biringi Sharks, klabu inayoshiriki ligi ya kaunti ya Kilifi.