FATUMA ZARIKA ASHAURI SERIKALI KUHUSU NDONDI

Bondia wa kike hapa nchini Kenya Fatuma Zarika ameiomba serikali kuwekeza hata zaidi katika mchezo wa ndondi ili kuwezesha kuwepo kwa mabondia wengi hapa nchini tofauti na hali ilivyo kwa sasa.

Zarika ameomba serikali kuwezesha mchezo huo kuandaa mashindano mengi ili kuufanya mchezo huyo kuwa na mashabiki wengi pamoja na kuepusha mabondia kuumizwa na umaskini.

Amesema mabondia wengi nchini wanakosa kushiriki mechi au kupoteza matumaini kabisa kujiendeleza katika ndondi kutokana na ukosefu wa ajira hivyo ukosefu wa fedha unawafanya kudhalilika licha ya kwamba wako na uwezo wa kuandikisha historia katika taifa hili.

Zarika wikendi iliyopita alipambana na Conjestina Achieng katika pigano lililofanyika katika kaunti ya Mombasa, pigano ambalo liliandaliwa na Mike Mbuvi Sonko.