SHABANA NA MURANG’A SEAL ZAREJEA KPL

Klabu ya Shabana sasa imepanda daraja kutoka ligi ya National Super League hadi ligi kuu ya fkf nchini baada ya kusajili ushindi wa bao 1-0  jana dhidi ya klabu ya Migori Youth.

Klabu ya Shabana imekuwa nje ya ligi kuu ya fkf kwa kipindi cha miaka 17 na  msimu huu wanalenga kupanda kwa kishindo kwani bado wako mbioni kushinda taji la ligi ya National Super League.

Shabana ambayo ni klabu ya jamii, mashabiki wake wanatoa shinikizo kwa wakuu pamoja na wachezaji wa klabu hiyo kutoachilia taji la National Super League licha ya kuthibitisha nafasi yao ya ligi kuu ya fkf msimu ujao.

Klabu ya Muranga Seal nayo imepata nafasi ya kupanda hadi ligi kuu ya Kenya Premeir league kutoka National Super League baada ya jana kusajili ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Heros katika uwanja wa Mbaraki Sports club jijini Mombasa.