UKOSEFU WA FEDHA WAUMIZA INTER DABASO

Klabu ya Kamtonga kutoka Taita Taveta, klabu inayoshiriki katika ligi ya daraja la pili kitaifa wikendi hii ilipewa alama tatu na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Klabu ya Inter Dabaso kukosa kuheshimu ratiba.

Inter Dabaso kutoka watamu kaunti ya Kilifi, klabu inayoongozwa na mkufunzi Sammy Randu ililazimika kukosa mechi hiyo kutokana na changamoto ya usafiri pamoja na hela za kulipa waamuzi wa mechi hiyo.

Hayo yakijiri vilabu vya mashinani vinazidi kutoa wito kwa jamii kudhamini vilabu huku FKF ikiombwa kutafuta mikakati ya kusaidia vilabu vinavyohiriki katika ligi.

Matokeo ya FKF daraja la pili kitaifa wikendi hii ni;

  1. Ashton Rangers vs Omax 3-1
  2. Ziwani Youth vs Sango Sportiff 1-0
  3. Beach Bay vs Samburu Lions Fc 0-0
  4. Sparki Youth vs Kishada fc 1-0