Kelly Maestro ambaye ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Samburu Lions analalamikia kucheleweshwa kwa kuachiliwa na klabu yake ya zamani kipindi ambacho sasa anafaa kujiunga na klabu ya Omax Fc kutoka kaunti ya Mombasa.
Kelly alitia saini katika klabu ya Omax lakini Samburu Lions kukosa kuachilia stakabadhi zake ndio jambo linalomfanya kukosa kushiriki mechi za Omax.
Mchezaji huyo kutokana na kukosa kucheza jambo linalochangia kuwa na hali ngumu ya kiuchumi amelazimika kurejea nyumbani kwao Malindi Kaunti ya Kilifi.

