MATAYARISHO YA MASHINDANO YA BODABODA YANANOGA MALINDI

Muungano wa bodaboda mjini Malindi kaunti ya Kilifi unazidi unazidisha maandalizi ya mashindano ya soka yatakayofanyika siku ya jumamosi katika uwanja wa Alaskan.

Ni mashindano ambayo yanalenga kuhamasisha wafanya biashara ya bodaboda kuhusu sheria za barabarani, usalama wao pamoja na kuwahamasisha kuhusu bishara hiyo ambayo imeajiri vijana wengi hapa nchini.

Akizungumza na Tama la Spoti kupitia njia ya simu John Randu ambaye ni mwenyekiti wa bodaboda amesema kwamba mashindano hayo yanalenga kuhusisha timu nane.

” Kwa saa hii tumepata timu nane ambazo zimethibitisha kwamba zitashiriki katika mashindano hayo siku ya Jumapili. Mashindano hayo yataanza saa 2.00 asubuhi na kutamatika masaa ya jioni.”

Timu nne za wanajamii ni timu ya Mogo ambayo pia ni wadhamini wa mashindano hayo kutokana na kwamba wamekuwa wakikopesha vijana wengi pikipiki za bodaboda, wachezaji wakongwe, timu ya jamii ya wakongo wanaoishi Malindi pamoja na walimu.