Waziri wa michezo Ababu Namwamba ameeleza kufurahishwa kwake na jinsi serikali ya William Ruto inavyotuza wanamichezo wa Kenya baada ya kufanya vyema katika michezo ya kimataifa wakiwakilisha taifa hili.
Ameyasema hayo baada ya rais William Ruto kuja na mpango uliomfanya Faith Kipyegon kutunukiwa nyumba ya milioni sita pamoja na kitita cha milioni pesa taslimu za Kenya baada ya kuandikisha rekodi mbili za kihistoria katika mashindano mawili makubwa katika kipindi cha wiki moja.
‘’Tunamtuza Faith Kipchoge kima cha shilingi milioni tano kwa kuvunja rekodi ya mita 1500 pamoja na nyumba ya shilingi milioni 6 kwa kuvunja rekodi ya pili ya mita 5000’’ Alisema Ruto
Ababu amepongeza hatua hiyo kwa kusema kwamba itachochea wachezaji wengine wa Kenya kujituma zaidi katika kuliwakilisha taifa la Kenya.
Waziri huyo amethibitisha kweli taifa la Kenya linatambulika kimataifa kutokana na mchango wanaouleta wanariadha pamoja na wanamichezo wengine wanaposhuka viwanjani katika arena za kimataifa.
‘’Tumetangaza kwamba, mchezaji yeyote atakayevunja rekodi ya kimataifa atakuwa anapewa shilioni tano. Kuanzia sasa tunawapa heshima kwa kutuheshimisha katika anga za kimataifa. Hii ni kati ya mpango mpya wa kuwapa motisha wachezaji wa Kenya ili wazidi kujituma zaidi uwanjani’’ Aliongeza Ruto.

