HARAMBEE STARS YASHINDA MECHI YA KWANZA

Timu ya taifa ya kenya  Harambe Stars imesajili ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Pakistan katika mashindano ya mataifa manne yanayoendelea nchini Mauritious.

Bao la pekee na la ushindi la Moses Shumah ambaye anachezea klabu ya Kakamega Homeboyz hapa nchini  kunako dakika ya 44 ndilo lilitosha kuwapa ushindi vijana hao wa Kenya.

Kwa sasa Harambee Stars wanasubiri kucheza mechi yao ya mwisho kati ya Mauritious siku ya jumapili kabla kurejea nchini baada ya kukosa mechi yao ya kwanza wikendi ilopita kwa kukosa usafiri wakati uliofaa.

Wikendi iliyopita (Jumapili) Harambee Stars walivaa kucheza dhidi ya timu ya taifa ya Djibouti lakini walifeli kutokana na kukosa ndege ya kusafiri hadi taifa hilo. Taarifa hiyo ilitolewa na katibu wa soka la Kenya Barry Otieno.