Kipa wa taifa la Poland Wojciech Szczęsny ni rasmi sasa amekamilisha vipimo vya kiafya tayari kwa kujiunga na klabu ya Barcelona.
Taarifa za usajili wake zilikuja baada ya kipa nambari moja wa Barca Marc-André ter Stegen kupata jeraha ambalo limekisiwa kuwa huenda likawa la muda mrefu.
Szczęsny ambaye zamani alikuwa akiichezea klabu ya Juventus pamoja na Arsenal amelazimika kukubali kukatwa mshahara katika dili la uhamisho ambalo limehusisha mkataba wa mpaka mwezi juni 2025.
Szczęsny anatarajiwa kuwajibishwa katika kikosi cha mkufunzi Hansi Flick hii leo usiku dhidi ya Young Boys kwenye michuano ya Uefa Champions league.