Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe anatarajiwa kukosa kusafiri kuelekea kwao kwa ajili ya mashindano ya mapumziko ya kimataifa
Mbappe ambaye alishiriki mechi ya Uefa jana licha akiwa bado na mashaka ya majeruhi imethibitika kuwa atasalia Madrid.
Kulingana na taarifa ni kuwa Mbappe atasalia Madrid kuendelea kupata nafuu ya jeraha lake. Jana Mbappe alijumuishwa kwenye kikosi cha Uefa kilichopigwa bao 1-0 na klabu ya Lille ya Ufaransa
Wengine wa Ufaransa ambao hawtakuwa safarini ni pamoja na Adrien Rabiot pamoja na Ferland Mendy ambaye yuko na Jeraha
Mchezaji mpya wa Chelsea Christopher Nkunku anatarajiwa kuhusishwa kwenye kikosi hicho cha kocha Didier Deschamps

