WAZITO FC YAMPA KAZI NKATA

Klabu ya Wazito FC hii leo imempa kazi ya ukufunzi mkuu Paul Nkata raia wa Uganda kuchukua nafasi ya Jaffers Odongo ambaye aliachana na klabu hiyo na kujiunga na Kakamega Homeboys kuwa msaidizi wa mkufunzi mkuu.

Kulingana na taarifa za majarida kadhaa nchini Kenya ni kwamba mkufunzi Nkata tayari yupo nchini na ataanza majukumu yake katika mechi ijayo Wazito FC watakapokuwa wanashuka dimbani dhidi ya klabu ya Bandari fc.

Ikumbukwe kwamba Nkata aliwahi kuiongoza Tusker kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya fkf mwaka wa 2016 kabla ya kuhamia klabu ya Kakamega Homeboyz ambako mmiliki wa klabu hiyo alimfuta kazi mwaka 2019 baada ya kutoka kwa madai kwamba Nkata amehusika katika suala la upangaji wa matokeo.