BENSON OMALA YWAIPEPERUSHA KOGALO

Benson Omala fowadi wa klabu ya Gor Mahia ameisaidia timu yake kuishinda Wazito FC katika dimba la Kasarani na kupanda hadi nafasi kwanza katika ligi kuu FKF.

‘Hatrick’ ya Omala ambaye ni mchezaji wa zamani wa Western Stima katika ingwe ya kwanza ya mchezo wa leo pamoja na bao la John Ochieng ndiyo mabao yalitosha kuwapa ushindi vijana hao wa mkufunzi Johnnathan McKisntry.

Sasa Gor Mahia inaongoza ligi na alama 33 wakiwa na mechi moja kiporo na utofauti wa alama mbili mbele ya wanzasukari Nzoia Sugar.

‘Hatrick’ ya Omala msimu huu inaongeza idadi yake ya mabao hadi mabao 15 baada ya mechi 14.